Na Veronica Mwafisi-Arusha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekea tabia ya baadhi ya Waajiri kuwahamisha watumishi wanaowakuta katika Ofisi walizoteuliwa na kutaka wahamishiwe katika vituo vingine vya kazi.
Waziri Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 19 Februari, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha wakati akifunga rasmi mkutano wa sita wa Serikali Mtandao ulioanza tarehe 17 Februari, 2026.
Amesema kama ikitokea mtumishi ana tatizo lolote la kiutumishi linalohitaji hatua za kinidhamu, apelekwe kwenye vikao vya kinidhamu ili adhabu stahiki itolewe na sio kuwaonea watu kwasababu ya unyonge wao.

Nataka niwakumbushe kuwa, kila mmoja aliingia kwa sifa zake, wengine wameingizwa kupitia mitihani ya ajira, wengine kwa nafasi za uteuzi, hivyo kila mmoja akitimiza wajibu wake ni wazi kuwa matokeo mazuri yataonekana.
Aidha, amepiga marufuku watumishi wa umma kutumia barua pepe binafsi kutuma taarifa za ofisi badala ya kutumia barua pepe rasmi za serikali.
Ni changamoto kubwa sana, bado tunao watumishi wa umma wanaotumia mitandao binafsi kutuma taarifa rasmi za serikali, tunachokifanya ni jambo la hatari sana, tutumie mifumo yetu iliyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani, Mhe. Kikwete ameongeza.
Waziri Kikwete amewapongeza e-GA kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwasisitiza Waajiri kutumia wataalam hao kutengeneza mifumo katika taasisi zao.
Ametoa wito kwa wataalamu wa TEHAMA kuendelea kujifunza kila wakati ili waweze kukabiliana na changamoto mbambali ikiwemo shambulio la mifumo ya TEHAMA.
Akitoa salamu kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Waziri Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuishirikisha kamati hiyo. Mmetambua uwepo wa mhimili wa Bunge, mngeweza hata kufanya wenyewe bila hata ya kutushirikisha, ameongeza Mhe. Dkt. Ndumbaro.
Amesema yeye sio mtaalam wa TEHAMA, lakini bado anatambua umuhimu wa serikali mtandao na kuongeza kuwa, kwa dunia ya leo hatuwezi kusonga mbele bila ya TEHAMA.
Amesema, Tanzania imepata mafanikio makubwa ambayo yanatokana na kazi nzuri ya Serikali kupitia Chama Cha Mapinduzi pamoja, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).
“Sisi kama kamati na Bunge tunatambua mafanikio hayo. Mafanikio ya kupeleka huduma kwa umma, kunganisha mifumo, kutuhakikishia usalama mtandaoni ni kazi nzuri yenye mafanikio makubwa
Tuko tayari kushirikiana na Wizara kuhakikisha changamoto zinazohusu sera, sharia na bajeti zinafanyiwa kazi. Kila mawasiliano ya Bunge yanakwenda kwa mtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba amemshukuru Waziri Kikwete pamoja na uongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa maelekezo na msisitizo kuhusu uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwani vimeongeza uzito, mwelekeo na ari mpya kwa washiriki wote.
Tunathamini sana mchango wako na w viongozi wote katika kuendeleza ajenda ya mageuzi ya kidijitali Serikalini, Mhandisi Ndomba amesisitiza.

No comments:
Post a Comment