Na mwandishi wetu.
Mnamo tarehe 02.03.2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Kibondo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mh. Maila M. Makonya (PRM) na Mwendesha Mashtaka kutoka TAKUKURU Bw. Balamu Kisumo, limefunguliwa shauri la uhujumu uchumi Namba ECO.4485/2026 Jamhuri dhidi ya Bw.Perfect Slaa Heke (36) ambaye alikuwa muuguzi katika zahanati ya kisogwe.
Mshtakiwa anakabiliwa na kosa la Ubadhirifu na Ufujaji kinyume na kifungu cha 28(1) PCCA sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022 baada ya mshtakiwa kufanya Ubadhirifu wa dawa za binadamu zenye thamani ya Tshs. 5,381,379.069
Kwamba, mshtakiwa wakati akiwa muuguzi na mtunza dawa zahanati ya kisogwe alikuwa anaomba dawa kwenye zahanati mbalimbali ambazo aliziomba kwa matumizi ya zahanati ya kisogwe lakini alikuwa anatumia dawa hizo kwa maslahi yake binafsi.
Baada ya kusomewa shtaka lake, Mshtakiwa alikana shtaka na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama.
Shauri limepangwa tena tarehe 13.03.2026 kwa ajili ya uwasilishaji wa hoja za awali (PH)
TAKUKURU (W) KIBONDO Machi 2,2026


No comments:
Post a Comment