
Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, kwenye Kikao cha Bodi ya Wadhamini wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), kilichoketi leo tarehe 4 Machi 2026, Kibaha, mkoani Pwani.
Wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho ni; Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU-PF (Zimbabwe), Jacob Francis Nzwindamilimo Mudenda, Chama cha SWAPO (Namibia), kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dkt. Samuel Abraham Peyavali Mushelenga na Chama cha MPLA (Angola) kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederico Toth Jorge De Miranda.






No comments:
Post a Comment