MIRADI YA MAJI YAZIDI KUPOKEA FEDHA KUFIKISHA MAJI KWA WANANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 16, 2026

MIRADI YA MAJI YAZIDI KUPOKEA FEDHA KUFIKISHA MAJI KWA WANANCHI


Serikali imetoa kiasi cha Shilingi bilion 930 katika miradi ya Sekta Maji, ikiwemo Shilingi Bilion 336 kwa ujenzi wa Bwawa la Kidunda.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Angellah Kairuki (Mb) amesema hayo akizindua rasmi mdahalo unaohusu "Maji na Jinsia, kuangazia usawa katika upatikanaji wa huduma za maji na Rasilimali za Maji na kugharamia masuala ya Jinsia katika kuandaa na kutekeleza Miradi" mjini Morogoro ikiwa ni sehemu ya kuelekea Siku ya maji Duniani, Machi 22.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kabla ya ufunguzi huo amewashukuru wadau wote wa Sekta ya Maji kwa kuhudhuria na kushirikiana na Wizara ya Maji katika kufanikisha huduma ya maji kwa jamii.

Mhandisi Mwajuma amewataka washiriki wa mdahalo huo kubadilishana mawazo kwa kuangazia mikakati bora ya kuhakikisha rasilimali za maji zinatunzwa, pamoja na uandaaji wa sera na mipango itakayosaidia kufikia dhamira ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya "Kumtua mama ndoo kichwani" na kuendana na Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2050 kwa kuwafikia wananchi wote.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Mussa Kilakala, akiongea kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro ameipongeza Wizara ya Maji kwa ujenzi wa miradi ya maji ikiwemo bwawa la Kidunda ambalo litanufaisha mkoa huo kwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 190 pamoja na uwezo wa kuzalisha umeme megawati 20.

No comments:

Post a Comment