Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba, amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda nyumbani kwake, Zuzu – Dodoma, lengo likiwa ni kumuekeza Waziri Mkuu huyo mstaafu jinsi sekta ya ununuzi wa unma ilivyopata mafanikio.
Bw. Simba alimuelezea Waziri Mkuu huyo Mstaafu jinsi ambavyo sekta ya ununuzi wa umma imepata mafanikio baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kuwezesha uwepo wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 na kujenga Mfumo wa NeST.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu, sheria hii ya ununuzi wa umma imelenga kuhakikisha kuwa watanzania wote wenye makampuni na wasio na makampuni wanaweza kufaidika na fursa za ununuzi wa umma kama wazabuni, ili kuwe na uchumi jumuishi. Imewapa fursa za pekee watanzania kupitia upendeleo maalum, ambapo zabuni zote zenye thamani isiyozidi Shilingi Bilioni 50 zimetengwa kwaajili ya watanzania pekee,” alisema Bw. Simba.
“Lakini pia kuna dirisha la watanzania ambao hawana uwezo wa kufungua makampuni kwa sasa, ambapo wametengewa asilimia 30 ya bajeti yote ya ununuzi wa umma ambayo ni takribani Shilingi Trilioni 5, ambazo wanaweza kuzipata kupitia utaratibu wa kuunda vikundi vya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu na kuomba zabuni,” aliongeza.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu alieleza kuhusu mapinduzi yaliyotokana na uwepo wa Mfumo wa NeST, ambao umeongeza uwazi, uwajibikaji na haki. Pia, alisema Mfumo huo umepunguza muda wa michakato ya zabuni pamoja na gharama za michakato hiyo.
Alisema NeST imeondoa matumizi ya karatasi na hivyo kulinda mazingira na gharama za tona, huku wazabuni wakiondolewa gharama na adha ya kusafiri kwaajili ya kuwasilisha nyaraka kwenye taasisi nunuzi.
Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Pinda aliipongeza Serikali kupitia PPRA kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya ununuzi wa umma, akieleza kuwa suala la fursa kwa makundi maalum linapaswa kuongezwa nguvu zaidi kwa kutoa elimu na hamasa ili kufikia lengo la kuwainua kiuchumi wananchi wengi zaidi, hususan wa ngazi ya chini na ngazi ya kati.
“Hili suala la makundi maalum sio suala la taasisi moja, ni suala mtambuka kama ulivyosema Mkurugenzi Mkuu. Sasa tunatakiwa kuhakikisha kila kiongozi kwa ngazi zote hadi ngazi za Serikali za mtaa wanaelewa vizuri na kufanyia kazi. Pia, watanzania wapate elimu nzuri na hamasa. Na wale waliokwishapata zabuni watakuwa hamasa zaidi kwa wengine,” amesema Mhe. Pinda.
Mheshimiwa Pinda aliahidi kuwa sehemu ya hamasa kwa vikundi, akianza kwa kuhamasisha vikundi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa mkoa wa Dodoma.
Aidha, aliishauri PPRA kuhakikisha wazabuni wanapata elimu ya kutosha kuhusu ushiriki wa zabuni na utekelezaji wa mikataba ya zabuni ili waweze kutekeleza ipasavyo mikataba husika.

No comments:
Post a Comment