WAZIRI WA ULINZI NA JKT AMKABIDHI MKUU WA MAJESHI MSTAAFU MWAMUNYANGE NA MAJENERALI WASTAAFU MAGARI MAPYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 7, 2026

WAZIRI WA ULINZI NA JKT AMKABIDHI MKUU WA MAJESHI MSTAAFU MWAMUNYANGE NA MAJENERALI WASTAAFU MAGARI MAPYA


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), kwa niaba ya Rais ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 06 Machi, 2026, amewakabidhi magari mapya ya kisasa, Maafisa Jenerali Wastaafu wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange katika hafla iliyofanyika ofisi ndogo za Wizara Upanga Jijini Dar es Salaam.

Hafla ya kukabidhi magari hayo kwa maafisa jenerali wastaafu toka kwa Serikali ni moja wapo ya stahiki za Jenerali mstaafu katika utumishi wa Jeshi ambapo makabidhiano hayo ya magari ni utekelezaji wa mpango wa Serikali kuwabadilishia Majenerali wastaafu magari yaliyofikisha miaka kumi ya kutumika tokea yaliponunuliwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe Dkt. Rhimo Nyansaho amewashukuru na kuwapongeza Majenerali hao kwa mchango wao mkubwa na uliotukuka kwa Taifa la Tanzania, akawaambia kuwa wamelitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Taifa kwa ujumla kwa uzalendo wa hali ya juu wakati wa utumishi wao, hivyo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa hali ya Ulinzi na Amani tunayoifurahia leo ni matokeo ya misingi imara iliyowekwa na viongozi hao wastaafu. Hivyo, Waziri wa Ulinzi na JKT akawaambia Majenerali hao wastaafu kuwa kuwabadilishia magari hayo baada ya zamani kuchakaa ni kielelezo cha namna Rais Samia Suluhu Hassan anavyojali na kuthamini ustawi na heshima ya wale waliojitoa muhanga maisha yao kulinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Rhimo Nyansaho ameongeza kwa kuwaambia Majenerali hao kuwa, Serikali inahakikisha kuwa wastaafu hawa na wengine waliotumikia Taifa wanaendelea kuishi kwa heshima na utulivu, huku wakibaki kuwa hazina ya busara kwa jeshi lililopo kazini hivi sasa.

Akiongea kwa niaba ya Majenerali wastaafu waliokabidhiwa magari hayo mapya, Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuwajali na kuwapatia nyenzo hizo mpya za usafiri, akaahidi kwa niaba ya wastaafu hao.








No comments:

Post a Comment