ASKOFU BROWN MWAKIPESILE ATUNUKIWA UPROFESA WA HESHIMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 17, 2026

ASKOFU BROWN MWAKIPESILE ATUNUKIWA UPROFESA WA HESHIMA



Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Waumini wa dini ya Kikristo nchini wametakiwa kutumia majukwaa ya kidini kutoa ushauri wenye kujenga kwa Serikali badala ya kutumia lugha ya matusi na kejeli zinazokiuka sheria na kuhatarisha usalama wa taifa, huku viongozi wakisisitizwa kutenda haki na kulinda amani ili kudumisha umoja na utulivu wa nchi.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Balozi wa Amani nchini, Prof. Isack Yona wakati wa hafla ya kumtunuku shahada ya heshima ya udalisi katika uungu (Honorary Professorship in Divinity) ya Chuo Kikuu cha Harvest Mission International Texas, Amarillo, U.S.A 2026, Askofu Mkuu wa Makanisa ya EAGT Tanzania, Askofu Prof. Brown Mwakipesile.

"kuna namna nzuri tu ya kufikisha ujumbe au ushauri kwa Serikali bila kutumia lugha ya matusi au kejeli kwani tunapaswa kuhakikisha kuwa nia zetu ni safi wakati tunashauri maana nchi yetu inatutegemea Sote tuijenge kwa hekima bila kuumizana na kuhatarisha amani, " amesema Prof. Isack


Prof. Yona amesema ipo haja kwa jamii kuanza kuwajenga watoto katika misingi ya maadili, uzalendo na haki tangu wakiwa wadogo ili taifa liendelee kuwa na viongozi bora, wananchi wavumilivu na watu wanaochukia matendo maovu.


Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Makanisa ya EAGT Tanzania, Askofu Prof. Brown Mwakipesile amesema tuzo hiyo ni heshima kubwa kwake na itakuwa chachu ya kuendelea kulitumikia taifa na jamii kwa kuhubiri amani, mshikamano na maadili mema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Janeth Mayanja ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, amewataka viongozi wa dini kuendelea kuwa mabalozi wa amani kwa kuhubiri upendo, mshikamano na kuheshimu sheria za nchi ili kudumisha utulivu uliopo nchini.

Aidha, viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wameeleza kuwa malezi bora ya watoto na ushirikiano kati ya viongozi wa dini na Serikali ni msingi muhimu wa kujenga taifa lenye maadili na amani ya kudumu.











No comments:

Post a Comment