Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amewataka vijana, wafanyabiashara na makundi maalum nchini kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana katika zabuni za Serikali ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa.
Akifungua mafunzo ya fursa na haki za wafanyabiashara na makundi maalum katika michakato ya ununuzi wa umma yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma, Mhe. Senyamule amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha uwazi, uwajibikaji na thamani ya fedha katika sekta ya ununuzi wa umma.
Amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya kuwainua wananchi kiuchumi kupitia mifumo ya ununuzi wa umma inayowezesha wazabuni kushiriki kwa uwazi huku haki zao zikilindwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha, ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma kwa kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara, vijana na makundi maalum kuhusu fursa zilizopo katika zabuni za umma pamoja na namna ya kushiriki kikamilifu katika michakato hiyo.
Mhe. Senyamule amesema bado kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili watanzania wengi zaidi wapate uelewa wa sheria za ununuzi wa umma, haki zao pamoja na namna bora ya kushiriki katika zabuni za Serikali.

Amesema Dodoma imeendelea kuwa kitovu muhimu cha shughuli za kiuchumi na maendeleo, hali inayoongeza umuhimu wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara na vijana ili waweze kutumia vyema fursa zilizopo katika sekta ya umma.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kwa makini mada zinazowasilishwa ili kupata maarifa yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika zabuni za umma na kusaidia Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradi yake.

Pia ametoa rai kwa PPAA na PPRA kuendelea kuelimisha vijana kuhusu fursa za uwekezaji, biashara na uchumi wa ubunifu ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma, Bw. James Sando amesema mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa wa wafanyabiashara na makundi maalum kuhusu haki zao katika michakato ya ununuzi wa umma pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kushughulikia malalamiko na rufaa.
Bw. Sando amesema PPAA ni taasisi inayojitegemea chini ya Wizara ya Fedha yenye jukumu la kupokea na kusikiliza malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya ununuzi wa umma pamoja na masuala ya kufungiwa kwa wazabuni kushiriki katika zabuni za Serikali.
Amesema kutokana na maboresho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023, PPAA imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia malalamiko na rufaa kupitia Mfumo wa NeST tangu Februari 2025.
Amesema matumizi ya mfumo huo yameleta manufaa mbalimbali ikiwemo kuokoa muda, kupunguza gharama, kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi za malalamiko na rufaa zinazowasilishwa na wazabuni. Aidha, wazabuni sasa wana uwezo wa kufuatilia hatua za rufaa zao moja kwa moja kupitia mfumo huo wa NeST.
Bw. Sando amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, PPAA imefanikiwa kutoa elimu kwa wazabuni 1,296 pamoja na watumishi 705 wa idara za ununuzi na sheria katika maeneo mbalimbali nchini, huku vijana 878 wakipatiwa mafunzo maalum ya kudai haki zao katika michakato ya ununuzi wa umma.
Ameongeza kuwa PPAA ina mpango wa kuunganisha mfumo wa kushughulikia rufaa na malalamiko na mfumo wa Mahakama ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

No comments:
Post a Comment