SIDO YAHAMISHA TEKNOLOJIA NANE ZA UCHAKATAJI MAZAO, YAIMARISHA UBUNIFU WA VIWANDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 22, 2026

SIDO YAHAMISHA TEKNOLOJIA NANE ZA UCHAKATAJI MAZAO, YAIMARISHA UBUNIFU WA VIWANDA



Na Okuly Julius ,OKULY BLOG,DODOMA


WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Small Industries Development Organization (SIDO) imeendelea kuimarisha ubunifu, utafiti na maendeleo ya teknolojia kwa kufanikiwa kuhawilisha teknolojia nane za kuchakata mazao mbalimbali katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Hayo yameelezwa bungeni na Waziri wa wizara hiyo ,Mhe. Judith  Kapinga wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Waziri Kapinga amesema teknolojia zilizohawilishwa ni pamoja na teknolojia ya utengezaji wa kinu cha kuchoma masalia ya kilimo, mashine ya kutengeneza mkaa mbadala, mashine ndogo ya kusafisha mafuta ya alizeti pamoja na mashine za kuzalisha chakula cha samaki.

Teknolojia nyingine ni mashine za kusaga mawe yenye madini, mashine za kukamua na kuchuja mafuta ya nazi, mashine za kubangua korosho pamoja na utengenezaji wa cage za ufugaji wa samaki katika maziwa, mito na bahari.

Katika hatua nyingine, Waziri Kapinga amesema SIDO kwa kushirikiana na United Nations Industrial Development Organization (UNIDO) imetengeneza mashine tatu za kuzalisha mkaa mbadala sambamba na kuleta teknolojia mpya kutoka Japan kwa ajili ya uzalishaji wa kuni bora maarufu kama briquettes.

Amesema teknolojia hiyo imeanza kutumika katika maeneo ya Ifakara mkoani Morogoro Region, Kahama mkoani Shinyanga Region pamoja na Mwanjelwa mkoani Mbeya Region.

Aidha, amesema mitambo ya kuchuja madini na mchanga pamoja na kifaa cha kutoa mchanga kwenye mashimo ya madini imetengenezwa katika mikoa ya Lindi Region, Mbeya Region na Shinyanga Region.

Kwa mujibu wa Waziri Kapinga, hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya mazao, kukuza viwanda vidogo na kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji na uchakataji wa bidhaa nchini.

No comments:

Post a Comment