UWEKEZAJI WA MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI KUONGEZA UFANISI NA UWAZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 19, 2026

UWEKEZAJI WA MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI KUONGEZA UFANISI NA UWAZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na viongozi, na Watumishi wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC), mara baada ya kuwasili na kutembelea miradi mbalimbali ya kituo hicho Mei 18, 2026 jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisalimiana na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo Jijini Dodoma
Menejimenti na Watumishi wa Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba (hayupo pichani) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kuhusu utendaji wa kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) kilichopo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzungumza nao katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC) Jijini Dodoma.



Na. Antonia Mbwambo-Dodoma


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema uwekezaji wa matumizi ya Mifumo ya Tehama Serikalini utasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza ufanisi na Uwazi wa huduma zinazotolewa na Watumishi wa umma kwa wananchi kwa maslahi ya Taifa

Mhe. Qwaray ameyasema hayo Mei 18, 2026 wakati akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (eGovRIDC), Menejimenti pamoja na Watumishi kutoka Taasisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) mara baada ya Naibu Waziri huyo kutembelea Kituo hicho Jijini Dodoma.

“Ni lazima tufahamu kwamba, katika dunia ya sasa, mageuzi ya kidijiti si chaguo tena bali ni msingi wa ufanisi wa Serikali, ushindani wa kiuchumi na maendeleo ya kijamii”. Mhe. Qwaray alisema.

Amesema,Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, kupunguza urasimu na rushwa, kuongeza uwazi, na kurahisisha upatikanaji wa huduma za wananchi popote walipo.

Mhe.Qwaray ameongeza kuwa, Serikali imepata mafanikio makubwa katika matumizi ya mifumo ya Kidijiti katika Sekta mbalimbali ikiwemo kuongeza uwajibikaji, kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuboresha utendaji kazi wa Utumishi wa Umma.

Aidha, Mhe Qwaray amesema kituo hicho kimekuwa na mchango chanya katika matumizi ya Mifumo mbalimbali kama vile Mfumo wa wa kielektroniki unaoiwezesha Serikali kupokea na kushughulikia malalamiko, maoni, pongezi, na maulizo kutoka kwa wananchi kwenda kwenye taasisi zote za umma (e-Mrejesho) pamoja na Mfumo wa Dirisha la Huduma za Serikali ikiwemo tangazo la Gazeti la Serikali na Utoaji wa Vibali vya Likizo bila Malipo.

Mhe. Qwaray ametoa wito kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)
kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, Vyuo Vikuu, taasisi za tafiti pamoja na Sekta Binafsi ili tafiti zinazofanyika ziweze kutatua changamoto halisi za wananchi na taasisi za umma.

Vilevile ameitaka Taasisi hiyo kusimamia utekelezaji wa Sheria, Kanuni, na Miongozo ya Serikali Mtandao ili mifumo yote inayotengenezwa iwe salama, yenye kuwasiliana na mifumo mingine na kuleta tija kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba, amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ilianzisha Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Maendeleo ya Serikali Mtandao (e-GOVRIDC) kwa lengo la kuratibu shughuli za kitafiti, kubuni na kuendeleza jitihada za Serikali Mtandao, ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma kwa umma, kuwajengea uwezo na kukuza vipaji vya vijana wabunifu katika eneo la TEHAMA. 

Mhandisi Ndomba amemshukuru Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray kwa kuitikia wito wa kutembelea kituo hicho na kuahidi kwamba wameyapokea na wataenda kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi huyo. 

No comments:

Post a Comment