Na Oscar Assenga,TANGA
>Yalenga Kuimarisha Ufanisi wa Chama
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimeongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wake wa ujenzi wa nyumba 36 za watumishi baada ya Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Rajab Abdulrahman, kukabidhi shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo unaotekelezwa katika wilaya tisa za mkoa huo.
Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Mfaume Kizigo, katika hatua inayodhihirisha dhamira ya chama ya kuboresha mazingira ya kazi na makazi kwa viongozi wake wa ngazi za wilaya.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Rajab alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba mwaka huu na kwamba utakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha utendaji wa watumishi pamoja na shughuli za chama katika maeneo mbalimbali ya mkoa.
Alieleza kuwa mradi huo una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.5, huku fedha zote zinazohitajika kwa ajili ya utekelezaji wake zikiwa tayari zimepatikana kupitia michango ya wanachama, viongozi na wadau mbalimbali wa chama.
"Mradi huu unagharimu jumla ya shilingi bilioni 2, milioni 500 na laki 250. Fedha hizi zimepatikana kupitia michango mbalimbali ikiwemo milioni 56 zilizotolewa awali, milioni 10 kutoka kwa MNEC pamoja na michango iliyokusanywa kutoka wilaya zote za mkoa," alisema Rajab.

Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa kukamilika kwa nyumba hizo kutasaidia kutatua changamoto za makazi kwa baadhi ya viongozi wa chama katika ngazi ya wilaya, jambo litakaloongeza utulivu wa kazi, uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Alisema nyumba hizo si tu kwamba zitakuwa makazi ya viongozi, bali pia ni uwekezaji wa muda mrefu wa chama katika kujenga taasisi imara yenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuendelea kuwahudumia wanachama wake.

"Tunajenga misingi ya chama kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Viongozi wanaweza kubadilika, lakini miundombinu tunayojenga leo itaendelea kulitumikia chama kwa miaka mingi ijayo," alisisitiza.
Rajab aliongeza kuwa ujenzi wa chama ni jukumu endelevu linalohitaji mshikamano wa wanachama wote, akisisitiza kuwa maendeleo ya chama hayawezi kupatikana bila ushiriki wa pamoja wa wanachama wake.

Kutokana na hilo, aliwataka wana-CCM wa Mkoa wa Tanga kuendelea kuchangia kwa hali na mali, kutumia elimu na uzoefu wao pamoja na nguvu kazi katika kukiimarisha chama.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Mfaume Kizigo, alisema mradi huo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa chama wa kuimarisha utendaji wake katika ngazi za wilaya kwa kuhakikisha viongozi wanapata mazingira bora ya kazi na makazi.
Alifafanua kuwa kila wilaya imepangiwa kujenga nyumba nne ambazo zitatumika na viongozi muhimu wa chama na jumuiya zake.

"Kila wilaya imepangiwa kujenga nyumba nne ambazo ni nyumba ya Katibu wa CCM wa Wilaya, nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Vijana, nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Wazazi pamoja na nyumba ya Katibu wa UWT," alisema Kizigo.

Alieleza kuwa uwepo wa nyumba hizo utasaidia kupunguza gharama za upangaji wa makazi, kuimarisha upatikanaji wa viongozi katika maeneo yao ya kazi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za chama na jumuiya zake.
Kwa mujibu wa Kizigo, kukamilika kwa mradi huo kutakuwa hatua muhimu katika kuijengea CCM Mkoa wa Tanga miundombinu imara itakayosaidia kuendeleza shughuli zake za kisiasa, kiutawala na kijamii kwa ufanisi zaidi katika miaka ijayo.

No comments:
Post a Comment