DAWASA, JIJI, TARURA WAZIBUA MITARO YA MAJI TAKA INAYOZUNGUKA SOKO LA KARIAKOO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 10, 2026

DAWASA, JIJI, TARURA WAZIBUA MITARO YA MAJI TAKA INAYOZUNGUKA SOKO LA KARIAKOO.

Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Halmashauri ya Jiji ya Dar es Salaam wameshirikiana kuzibua mitaro ya maji taka inayozunguka Soko Kuu la Kariakoo.

Akizungumza baada ya zoezi la uzibuaji wa mitaro hiyo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim amesema zoezi hilo linafanyika kufuatia maelekezo aliyoyatoa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo kuwa taasisi hizo zikutane na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo na kuondoa kero kwa wananchi.

CPA. Abdukarim amemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya na wakuu wa taasisi hizo kwa namna waliyoshughulikia changamoto hiyo na kutuma wataalam wao kufika katika maeneo hayo, kitendo ambacho kwa pamoja kimefanikisha kutekelezeka kwa maagizo ya Mhe. Mkuu wa Wilaya.

Amesema shirika litaendelea kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha kuwa maeneo yanayolizunguka soko yanakuwa safi muda wote japo ambalo litachangia kuzuia kutokea kwa magonjwa ya mlipuko na pia wafanyabiashara kufanya biashara katika mazingira safi na ya kuvutia.

Soko Kuu la Kariakoo limejipambanua kwa usafi ambapo limeweka wafanya usafi katika maeneo ya kutolea huduma kitu kilichofanya soko hilo liwe safi na nadhifu muda wote huku likiwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara pamoja na wateja wanaoingia kila siku.

No comments:

Post a Comment