KAZI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI MWANZA YAANZA USIKU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 15, 2026

KAZI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI MWANZA YAANZA USIKU


Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), almeanza kazi ya kutatua changamoto ya huduma ya maji Jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo, Juni 15, 2026.

Mara baada ya kuwasili Mwanza usiku Waziri Aweso alifika katika Kituo cha Kusukuma Maji cha Capripoint na khongoza kikao cha dharura na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), kabla ya kwenda kukagua hali ya upatikanaji wa huduma ya maji jijini humo alfajiri.

Lengo la kikao hicho kililikuwa kupata picha halisi ya hali ya huduma ya maji, kubaini changamoto zinazowakabili wananchi, na kuandaa mpango wa hatua za haraka na za kudumu za kuboresha huduma hiyo.

Baada ya kukagua kituo hicho, Waziri Aweso aliagiza wataalamu wa Wizara ya Maji na MWAUWASA kukesha usiku kucha wakifuatilia na kuhakikisha upatikanaji wa maji unaimarika katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Aidha, ameahidi leo kutembelea maeneo kadhaa kujionea hali halisi, ikiwemo chamzo kikuu cha mani cha Butimba.

No comments:

Post a Comment