MKUTANO WA WENYE DHAMANA YA UCHUKUZI, UJENZI NA MAWASILIANO WAFANYIKA ZIMBABWE; CP KAGANDA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 29, 2026

MKUTANO WA WENYE DHAMANA YA UCHUKUZI, UJENZI NA MAWASILIANO WAFANYIKA ZIMBABWE; CP KAGANDA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA.


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Jamhuri ya Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, ameongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Tanzania kushiriki Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya Uchukuzi, Ujenzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika jijini Bulawayo, Zimbabwe.

Mkutano huo umeendelea nchini humo ukiwa na kaulimbiu isemayo “Anga Huria na Miundombinu Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi Inayowezeshwa na Akili Unde (AI) ili Kuharakisha Ushirikiano wa Kikanda na Maendeleo Endelevu katika SADC.”

Kabla ya mkutano wa Mawaziri, kulifanyika vikao vya wataalamu na Makatibu Wakuu Kwa upande wa Tanzania, ujumbe wa wataalamu uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde.

Mkutano huo umejadili na kufikia maazimio mbalimbali yanayolenga kuimarisha sekta za uchukuzi, ujenzi, mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na huduma za hali ya hewa, kwa lengo la kuharakisha ushirikiano wa kikanda na kuchochea maendeleo endelevu katika nchi wanachama wa SADC.

No comments:

Post a Comment