Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Juni 5, 2026, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.”
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mercy Kiamba, amesema ofisi hiyo inaendelea kutoa mchango mkubwa katika juhudi za uhifadhi wa mazingira kupitia usimamizi wa mashauri mbalimbali yanayohusiana na ardhi na uhifadhi wa rasilimali za mazingira.
Ameeleza kuwa usimamizi wa sheria na utoaji wa ushauri wa kisheria katika masuala ya ardhi ni miongoni mwa nyenzo muhimu zinazosaidia kulinda mazingira na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za taifa.
Kiamba amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za umma, sekta binafsi na wananchi katika kutekeleza wajibu wa kutunza mazingira ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

No comments:
Post a Comment