Na Okuly Julius, OKULY BLOG - DODOMA
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi zaidi ya 150 katika kipindi cha siku tano tangu kuanza kwa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma.
Mbali na huduma hiyo, wakala huo umepokea zaidi ya wananchi 300 waliotembelea banda lake kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo tangu maadhimisho hayo yalipoanza Juni 16, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20, 2026, Afisa Sheria wa RITA, Emmanuela Mwingira, alisema huduma ya vyeti vya kuzaliwa imeendelea kuvutia wananchi wengi wanaofika katika banda hilo, huku wengi wakitumia fursa hiyo kupata nyaraka muhimu za kisheria kwa urahisi.
Mwingira alisema RITA imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanaofika katika banda hilo wanapata huduma kwa wakati na kwa ufanisi, sambamba na kuwapatia elimu kuhusu umuhimu wa kusajili matukio mbalimbali ya kiraia.
Aidha, alisema baadhi ya wananchi wamejitokeza kupata huduma za wosia, huku akieleza kuwa huduma hiyo ni muhimu katika kusaidia wananchi kupanga na kulinda mali zao kwa mujibu wa sheria.
Aliongeza kuwa wananchi wanaohitaji huduma za vyeti vya kuzaliwa wanapaswa kufika na nyaraka muhimu zinazohitajika ili kurahisisha mchakato wa kupata huduma hiyo.
Mwingira amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani kuendelea kutembelea banda la RITA katika maadhimisho hayo ili kupata huduma mbalimbali, ikiwemo usajili wa vyeti vya kuzaliwa, huduma za wosia na huduma nyingine za kisheria zinazotolewa na wakala huo kwa muda mfupi.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameendelea kuwa jukwaa muhimu kwa taasisi za umma kusogeza huduma karibu na wananchi na kutoa elimu kuhusu majukumu na huduma wanazozitoa.

No comments:
Post a Comment