TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA ELIMU KWA WANANCHI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 20, 2026

TUME YA UTUMISHI WA UMMA YATOA ELIMU KWA WANANCHI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Na Okuly Julius, OKULY BLOG –DODOMA


Tume ya Utumishi wa Umma imesema itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu na huduma zake ili kuongeza uelewa wa umma kuhusu haki na wajibu katika utumishi wa umma.

Hayo yameelezwa na Katibu Msaidizi, Idara ya Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma, Cornelia Mvula,wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, ambapo taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda lake kwa ajili ya kujifunza kuhusu shughuli mbalimbali za tume hiyo.


Mvula alisema wananchi wengi wamekuwa wakifika katika banda la tume kupata taarifa na ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utumishi wa umma, jambo linalosaidia kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za umma.

Alieleza kuwa utoaji wa elimu hiyo ni sehemu ya juhudi za tume kuhakikisha wananchi wanatambua nafasi yake katika kusimamia maadili, haki na taratibu za utumishi wa umma nchini.

Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kutumia fursa ya maadhimisho hayo kutembelea banda la Tume ya Utumishi wa Umma ili kupata elimu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu utumishi wa umma.

Tume ya Utumishi wa Umma ni taasisi inayojitegemea iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 294, Marekebisho ya mwaka 2019, ikiwa na jukumu la kusimamia na kuimarisha mifumo ya utumishi wa umma nchini.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamewakutanisha taasisi mbalimbali za serikali zinazotoa huduma kwa wananchi, yakilenga kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza uelewa kuhusu majukumu ya taasisi hizo.

No comments:

Post a Comment