SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI-PROF.SHEMDOE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 9, 2026

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI-PROF.SHEMDOE


Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe.Prof.Riziki Shemdoe, amesema kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha miundombinu ya michezo nchini, ili kuendelea kukuza sekta hiyo.

Prof.Shemdoe amesema hayo leo tarehe 9 Juni 2026 Mjini Iringa, wakati akizungumza katika ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanayofanyika Kitaifa Mkoani humo.

Amesema kuwa lengo la kuimarisha miundombinu ni kuhakikisha kuwa vipaji vinavyoibuliwa havipotei, na vinaendelezwa kwa ajili ya kuja kulitumikia Taifa kupitia team mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

"Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa michezo na Sanaa inapewa kipaombele katika shule,kwa michezo ni uchumi iwapo itawekeza msingi mzuri" amesisitiza Prof.Shemdoe.

Awali akitoa salam za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Henry James alisema kuwa mashindano hayo ni fursa kwa wananchi ambao watapata nafasi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Alisema Mkoa huo umejipanga kwa ajili ya kuwahudumia wageni zaidi ya elfu 10 watakaohusika katika mashindano ya mwaka huu.

"Wananchi wa Iringa tumepewa heshima hii ya kuandaa mashindano hayo tangu mwaka jana, tunawahakikishia kuwa huduma zote muhimu zinapatikana wakati wowote hivyo wageni wote waendelee kufurahia michezo inayoendelea" alisema

No comments:

Post a Comment