SERIKALI YAENDELEA KUHAMASISHA UTAFITI, YATENGA SH. BILIONI 1.5 KWA TUZO ZA UMAHIRI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 18, 2026

SERIKALI YAENDELEA KUHAMASISHA UTAFITI, YATENGA SH. BILIONI 1.5 KWA TUZO ZA UMAHIRI


Na Boniphace John -Dodoma


Serikali kupitia Wizara ya elimu,Sayansi na Teknolojia Katika mwaka wa fedha 2026/2027 imetenga billion 1.5 kwa ajili ya tuzo ya umahiri kwa watafiti na wahadhiri kutoka taasisi za elimu ya juu za Serikali na zisizo kuwa za kiserikali.

Wizara hiyo imetangaza dirisha la kupokea machapisho ya watafiti wanaotaka kushindania tuzo hiyo ambalo litakua wazi kuanzia juni 16 mpaka Oktoba 31 mwaka huu.

Akizungumza leo na vyombo vya habari Jijini Dodoma Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema nyanja za ushindani zitakazo shindaniwa ni Sayansi asilia na Hisabati,Afya na Sayansi shirikishi,Sayansi za wanyama na kilimo pamoja na Uhandisi na Teknolojia ya habari na mawasiliano.

"Mtakumbuka Machi 26 mwaka 2023 serikali ilizindua tuzo ya umahiri kwa tafiti na wahadhiri kutoka taasisi za elimu ya juu za Serikali na ambazo sio za serikali na tuzo hutolewa kwa tafiti na wahadhiri hao ambao matokeo ya tafiti zao yanakuwa yamechapishwa katika majarida ya kitaaluma yenye hadhi ya juu duniani.

"Tuzo hii utolewa kwa fedha taslimu million hamsini(50) za kitanzania kwa kila chapisho moja na kugawanywa kulingana na mchango wa walioshiriki katika kufanya utafiti huo,"amesema Mkenda 

Amesema Utoaji wa tuzo hiyo ni moja ya mikakati ya serikali ya kukuza na kuendeleza Sayansi na Teknolojia hapa nchini na ni motisha kwa watafiti kukuza umahili na kuwa katika viwango vya juu vya kimataifa na viwango vya juu vya kimataifa vinapimika kirahisi sana kwasababu majarida haya yanafahamika duniani,yanafahamika jarida gani lipo juu kuliko mengine kwahiyo mtafiti anayefanya utafiti unaokubalika na kutambulika zaidi duniani kwa kawaida atakua amechapisha katika majarida ambayo ni ya juu zaidi.

Aidha ameeleza Tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo jumla ya machapisho 336 yalikidhi vigezo na kuingia katika ushindani katika machapisho hayo 86 yalipata tuzo watanzania 200 wameshinda tuzo hii tangu kuanzishwa kulingana na mchango wao katika machapisho yaliyoshinda.

No comments:

Post a Comment