Mhe. Wanu ametoa rai hiyo Juni 6, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha Superdoll, ambapo amehimiza utoaji wa elimu inayojikita katika ujuzi na umahiri ili kuwajengea wahitimu uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na kuendana na mahitaji ya sekta za uzalishaji.
Mhe. Ameir ameeleza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo 105 vya VETA na kuboresha vingine 12, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaohitajika katika uchumi unaobadilika.
Mhe. Wanu ameendelea kuzihimiza taasisi na wadau wengine kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kufungua milango ya mafunzo ya vitendo kwa vijana na wakufunzi ili kupunguza pengo kati ya maarifa ya darasani na ujuzi unaohitajika sokoni.
Aidha, ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuharakisha utiaji saini wa makubaliano na Kampuni ya Superdoll ili kuimarisha zaidi mafunzo ya vitendo kwa vijana.
Meneja wa Superdoll Bw. Ibrahim Ali amesema kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na taasisi za elimu, hususan VETA, ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mafundi wake, huku takribani asilimia 80 ya mafundi wa kampuni hiyo wakiwa wahitimu wa VETA. Ameongeza kuwa hivi karibuni kampuni imepokea vijana 20 kwa ajili ya tawi lake la Dodoma.
Naibu Waziri ameiagiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kutambuliwa rasmi Kituo Maalumu cha Mafunzo (Center of Excellence) cha Superdoll katika kukuza ujuzi na kuongeza uzoefu wa kazi kwa vijana wa Tanzania.










No comments:
Post a Comment