WITO WATOLEWA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA OWM MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 19, 2026

WITO WATOLEWA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA OWM MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI


Na Mwandishi Wetu-DODOMA


Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kupitia Wakala wa Serikali wa Uchapaji Tanzania inawaalika wananchi kutembelea Banda la Ofisi hiyo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo uchapishaji wa Sheria, Kanuni, Katiba ya Tanzania, machapisho mbalimbali ya vitambulisho vitambulisho, vyeti na nyaraka zote za kiserikali.

Wito huo umetolewa leo tarehe 19 Juni, 2026 katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma na Afisa Biashara Bi. Witness Njunde kutoka Wakala wa Serikali wa Uchapaji Tanzania wakati akizungumzia kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala huyo wa Serikali.

Bi. Njunde amesema “Moja ya kazi tunazofanya ni kuchapisha gazeti la Serikali, Gazeti hili la Serikali limebeba maudhui ambayo ni ya kiserikali na kibinafsi. Katika maudhui ya kibinafsi huwa linatangaza mabadiliko ya majina, mirathi, kupotea kwa leseni za makazi, kufungwa kwa makampuni hali kadhalika pindi mtu anapopotelewa na vyeti vyake vya shule, passport, leseni zote hizo tunatangaza katika gazeti la serikali”.

Aidha, ameongeza kuwa, Gazeti hilo la Serikali huwa linatangazwa mara moja kwa wiki kila ijumaa na nakala laini ya gazeti hilo huwekwa katika tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.

No comments:

Post a Comment