APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUGHUSHI MKATABA WA MAUZO ILI ALIPE GHARAMA PUNGUFU ZA MAUZIANO SERIKALINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 21, 2026

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUGHUSHI MKATABA WA MAUZO ILI ALIPE GHARAMA PUNGUFU ZA MAUZIANO SERIKALINI



NA Mwandishi Wetu - Kilimanjaro


Julai 10, 2026, Ofisi ya TAKUKURU Kituo Maalum Holili - Kilimanjaro imefungua shauri la jinai namba 15436/2026, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Bw. Alex Alfred Alexander, Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Iwa.

Shauri hilo limefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mbele ya Mhe. Ally Mkama, Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania.

Bw. Alex ameshtakiwa kwa makosa ya Kughushi Nyaraka chini ya vifungu vya 333, 335(a) na 337, pamoja na Kuandaa Nyaraka za Uongo chini ya vifungu vya 342 na 337, yote yakiwa ni makosa chini ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16, Toleo la Mwaka 2023.

Akiieleza Mahakama, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Bw. Arnold Mafwele, amesema kuwa mnamo Machi 30, 2026, mshitakiwa alighushi mkataba wa mauzo ya kiwanja kwa kuonesha kuwa thamani ya mauziano hayo ni kiasi cha Tsh. 5,000,000/=, ilhali thamani katika mkataba halisi ni Tsh. 20,000,000/=.

Bw. Arnold Mafwele ameeleza zaidi kuwa mshitakiwa aliwasilisha mkataba huo wa kughushi katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Iwa, jambo lililopelekea kulipwa kwa ushuru pungufu wa mauzo ya ardhi Serikalini.

Mshitakiwa amekana mashtaka yote, na kwa kuwa amekidhi vigezo vya dhamana, yupo nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment