EWURA CCC YAWAHIMIZA WANANCHI KULIPA ANKARA ZA MAJI KWA WAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 1, 2026

EWURA CCC YAWAHIMIZA WANANCHI KULIPA ANKARA ZA MAJI KWA WAKATI


Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam 

Katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, leo Julai 1, 2026 EWURA CCC imeendelea kutoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lake.


Kupitia elimu hiyo, pamoja mambo mengine, wananchi wamehimizwa kulipia ankara za maji kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa huduma pamoja na kuchangia uendelevu wa utoaji wa huduma bora za maji.


Aidha, wananchi pia wamekumbushwa kuwa wanazo haki mbalimbali ikiwemo haki ya kupewa taarifa sahihi na watoa huduma za nishati na maji ikiwemo bei, taarifa za katizo la huduma na kushirikishwa katika usomaji wa mita za maji na umeme ili kuwa na bili zenye uhalisia. 


EWURA CCC inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake katika viwanja vya Julius Nyerere (Sabasaba) ili kupata elimu, na taarifa zaidi kuhusu huduma za nishati na maji kwa kipindi hiki cha Maonesho ya Sabasaba, hadi tarehe 13 Julai, 2026.


No comments:

Post a Comment