Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa juhudi za Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini licha ya changamoto linazokabiliana nazo katika Utekelezaji wa majukumu.
Kamanda Muliro ametoa pongezi hizo alipozuru Kijiji cha Mazingira cha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) tarehe 7/7/2026 katika sikukuu ya maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (sabasaba 2026)
"Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya, siku hizi malalamiko ya uchafuzi wa mazingira yamepungua sana sio sawa na hapo zamani hasa Maeneo ya Mbagala." Alipongeza Kamanda Muliro
Aidha ametoa wito kwa Baraza kuongeza nguvu katika eneo la Utoaji elimu ya Mazingira kwa umma na kuongeza matangazo ili Jamii ipate uelewa mpana kuhusu Ulinzi na Uhifadhi wa Mazingira.
Kamanda Muliro pia amewatembelea wadau wote wa Mazingira wanaoshiriki maonesho katika Kijiji cha Mazingira na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuibua Teknolojia zinazoibua Fursa za kiuchumi na kuhifadhi Mazingira hasa katika eneo la urejelezaji wa taka.






No comments:
Post a Comment