Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira kabla ya kushiriki matembezi yaliyolenga kuhamashisha jamii katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira yaliyofanyika Julai 19, 2026 jijini Dar es Salaam.
*************
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kuimarisha juhudi za kuhakikisha kuwa masuala ya uendelevu wa mazingira yanapewa kipaumbele katika ajenda ya maendeleo ya Taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, aliposhiriki matembezi yaliyolenga kuhamashisha jamii katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ‘Save Soil Walkathon’ yaliyofanyika Julai 19, 2026 jijini Dar es Salaam.
Mhe Masauni amesema, ahadi hii inaonyeshwa wazi katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2050, haswa nguzo yake ya Tatu, ambayo inatambua uendelevu wa mazingira na ustahimilivu wa hali ya hewa kama misingi muhimu wa kufikia mabadiliko ya kiuchumi jumuishi ya kijani kibichi na endelevu.
Ameongeza kuwa afya ya udongo ni msingi wa usalama wa chakula, uhifadhi wa mazingira na ustawi wa uchumi wa taifa, hivyo kuna umuhimu wa kila Mtanzania kushiriki katika juhudi za kuutunza.
"Udongo ni rasilimali muhimu inayobeba maisha yetu ya kila siku. Bila udongo wenye afya hatuwezi kuwa na usalama wa chakula, mazingira bora wala maendeleo endelevu. Ni wajibu wa kila Mtanzania kushiriki katika juhudi za kulinda mazingira na kutumia ardhi kwa njia zinazohifadhi uhai wake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho," amesema Mhe. Masauni.
“Tunapoanza kutekeleza Mpango huu wenye kuleta mabadiliko makubwa, tunaona fursa nyingi za kuimarisha ushirikiano wetu na Jamhuri ya India. Tunatarajia kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama vile uhamishaji wa teknolojia, utafiti na uvumbuzi, ujenzi wa uwezo, urejeshaji endelevu wa ardhi, ufuatiliaji wa mazingira, uwekezaji rafiki kwa mazingira na suluhisho zinazozingatia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.” Amesisitiza Mhe. Masauni.
Kwa upande wake, Rais wa Lions Club of Dar es Salaam Mazingira, Bi. Lion Ramadevi, amesema ‘Save Soil Walkathon’ ni sehemu ya kampeni pana inayolenga kuhamasisha jamii kutambua mchango mkubwa wa udongo katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.
"Save Soil Walkathon si matembezi pekee, bali ni harakati ya kuhamasisha mabadiliko ya tabia na kuwajengea wananchi uelewa wa umuhimu wa kulinda udongo. Tunataka kuona jamii, taasisi na sekta binafsi zikichukua hatua za pamoja katika kuhifadhi mazingira kwa mustakabali wa taifa letu," alisema Lion Ramadevi.
Naye Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Lakshay Anand amesema ni jambo jema kuona jamii inatambua umuhimu wa kulinda mazingira na huo ndio msingi wa Maisha ya binadamu ya kuhakikisha kila mmoja anakua sehemu ya kutunza mazingira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira alipowasili eneo la Swami Vivekananda Culture Centre jijini Dar es Salaam kushiriki matembezi yaliyolenga kuhamashisha jamii katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira yaliyofanyika Julai 19, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akimwakilia maji mti mara baada ya kuupanda ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira, wakati aliposhiriki matembezi yaliyolenga kuhamashisha jamii katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira yaliyofanyika Julai 19, 2026 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akipanda mti ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira, wakati aliposhiriki matembezi yaliyolenga kuhamashisha jamii katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira iliyofanyika Julai 19, 2026 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati), akishiriki matembezi yaliyolenga kuhamashisha jamii katika Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira yaliyofanyika Julai 19, 2026 jijini Dar es Salaam.










No comments:
Post a Comment