
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na China katika diplomasia ya ulinzi ili kuimarisha usalama, maendeleo na uchumi endelevu wa mataifa hayo.
Dkt. Nyansaho amesema hayo tarehe 21 Julai, 2026, wakati wa maadhimisho ya miaka 99 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA), yaliyoandaliwa na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian.
Katika hotuba yake kwenye maadhimisho hayo, Waziri wa Ulinzi na JKT ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa China, Xi Jinping, kwa kuendeleza urafiki wa kihistoria ulioasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong, hususan katika sekta ya ulinzi.
Kwa upande wake, Balozi Chen Mingjian aliahidi kuwa China itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kihistoria na Tanzania katika masuala ya ulinzi, ikiwemo mafunzo ya kijeshi.







No comments:
Post a Comment