RAIS SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 25, 2026

RAIS SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 25, 2026 ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Uwanja wa Mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Rais Samia aliwasili katika viwanja vya maadhimisho na kupokelewa kwa heshima rasmi za kijeshi, kabla ya kupokea heshima ya wimbo wa Taifa la Tanzania na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika kilele cha maadhimisho hayo, Rais Samia aliweka mkuki na ngao kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya kutoa heshima kwa mashujaa waliojitolea kwa ujasiri na uzalendo kwa ajili ya Taifa.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, wanajeshi wastaafu, viongozi wa dini pamoja na wananchi na wageni mbalimbali.

Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa huadhimishwa tarehe 25 Julai ya kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka na kuwaheshimu mashujaa waliopigania uhuru wa nchi na wale waliojitolea kulinda amani, usalama na maslahi ya Taifa.

No comments:

Post a Comment