
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ameupongeza Uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (JUWATA) kwa maono yao mapana ya kutumia taaluma ya uandishi wa habari kama chombo cha kuhamasisha maendeleo ya jamii.
Amesema kuwa mbali na jukumu lao la kutoa habari kwa usahihi na weledi, wameonesha kuwa vyombo vya habari vinaweza pia kuwa washirika wakubwa katika kukuza uchumi wa wananchi kupitia elimu na mafunzo.
Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Beatrice Njawa wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tatu ya mafunzo ya Ujasiriamali ya "Jifunze kwa Mama Ujasiriamali" iiiyoanza Julai 13, 2026 kwenye Ukumbi wa Bwalo la JKT Umwema Mjini Morogoro.
Vilevile, amewapongeza MAMO Entrepreneurship kwa juhudi zenu za kuwainua wanawake, vijana na makundi mbalimbali kupitia mafunzo ya vitendo yanayowajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi. Serikali itaendelea kuthamini mchango wa taasisi kama hizi katika safari ya kujenga uchumi jumuishi.


No comments:
Post a Comment