SALOME MAKAMBA AUNGANA NA WADAU KATIKA MALEZI NA ULINZI WA WATOTO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 18, 2026

SALOME MAKAMBA AUNGANA NA WADAU KATIKA MALEZI NA ULINZI WA WATOTO


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Salome Makamba ametembelea na kutoa misaada kwenye makao maalum ya kulea watoto,ikiwa lengo ni kuunga mkono juhudi za wadau katika kulinda makundi ya watoto na kudhibiti hali ya mmomonyoko wa maadili unaendelea kuikumba jamii.
 
 Mhe. Salome amekabidhi vyakula mbalimbali pamoja mifuko 40 kwa vituo viwili vilivyopo Mjini Shinyanga ili kukamilisha hatua za ujenzi wa makazi hayo. 

Hata hivyo Mhe. Salome amesisitiza kuwa kuwepo kwa makazi hayo kutasaidia kudhibiti makuzi ya watoto katika suala la maadili, kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili pamoja na kuwapatia huduma muhimu ikiwemo Elimu,chakula,makazi na malazi.
 
 Katika hatua nyengine Mhe. Salome amekabidhi mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha uzio katika ujenzi wa nyumba ya makazi ya  katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment