Na Edward Winchislaus, OKULY BLOG, DODOMA
Serikali imezitaka taasisi za elimu ya juu na watafiti nchini kuhakikisha tafiti za afya zinazofanywa kwa kutumia fedha za umma zinatumika katika kufanya maamuzi ya kisera na kutatua changamoto za wananchi badala ya kuendelea kubaki kwenye makabrasha na machapisho ya kitaaluma.
Akifungua Kongamano la Tatu la Kisayansi la Afya la Chuo Kikuu cha Dodoma (USCHE) kwa niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya anayeshughulikia dawa na vifaa tiba, Dkt. Emanuel Tayari, amesema Bara la Afrika limekuwa na mtazamo usio sahihi kwamba fedha zinazowekezwa katika sekta ya afya ni matumizi, huku akisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeonesha kwa vitendo kuwa afya ni uwekezaji unaochochea ukuaji wa uchumi.
Amesema taifa lenye wananchi wagonjwa haliwezi kuwa na uchumi imara wala kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Dkt. Tayari amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta ya afya, ikiwemo kupungua kwa vifo vya wajawazito kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2020 hadi vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 mwezi Februari 2025.

Pia amesema vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka na kufikia 12,846 nchini, huku zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wakipata huduma karibu na maeneo wanayoishi kutokana na kuimarishwa kwa miundombinu na upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa.
Amesema changamoto iliyobaki ni matumizi hafifu ya matokeo ya tafiti licha ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Kutokana na hali hiyo, wizara imependekeza mfumo mpya wa ushirikiano na vyuo vikuu ambapo serikali itaweka wazi maeneo ya vipaumbele vya utafiti, kila utafiti unaofadhiliwa kwa fedha za umma uwe na muhtasari wa mapendekezo ya utekelezaji wa sera, huku makongamano yakihitimishwa kwa mapendekezo machache yanayoweza kutekelezwa mara moja.
Akizungumzia matumizi ya akili bandia katika sekta ya afya, Dkt. Tayari amesema teknolojia hiyo ni fursa muhimu ya kupunguza upungufu wa wataalamu wa mionzi na maabara, lakini imetakiwa kujengwa kwa kutumia taarifa za afya za Watanzania ili iweze kutoa majibu sahihi kwa mazingira ya nchini.
Amesema serikali haitaruhusu taarifa za afya za Watanzania kutumika bila usimamizi wa ndani na imevitaka vyuo vikuu kujenga uwezo wa kutengeneza mifumo hiyo nchini badala ya kutegemea teknolojia kutoka nje.
Aidha, ameitaka UDOM kuandaa mpango wa ushirikiano wa tafiti za afya utakaoshirikisha nchi nane jirani ili Tanzania iwe kitovu cha tafiti za afya barani Afrika, huku akisisitiza kuwa tafiti zinapaswa pia kuunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha dawa, chanjo na vifaa tiba nchini.

Awali, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri elekezi, Prof. Razack Lokina, amesema kongamano hilo lenye kaulimbiu "Afya Yetu, Mustakabali Wetu: Kujenga Mfumo Imara, Shirikishi na Endelevu wa Afya" limekusanya wataalamu wa afya, watafiti na watunga sera kujadili suluhisho la changamoto zinazoikabili sekta ya afya.
Amesema UDOM imeendelea kuzalisha wataalamu wa afya na kushirikiana na Hospitali ya Benjamin Mkapa katika kutoa huduma za kibingwa na bingwa bobezi, zikiwemo huduma za uchujaji damu na upandikizaji wa figo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof.Abel Makubi, amesema kongamano hilo litatoa nafasi ya kubadilishana uzoefu, kuwasilisha matokeo ya tafiti na kuibua ubunifu utakaoimarisha huduma za afya nchini na barani Afrika.
Amesisitiza kuwa wakati umefika kwa matokeo ya tafiti kutumika kutatua changamoto za wananchi na kuboresha utoaji wa huduma badala ya kuendelea kubaki kwenye nyaraka za kitaaluma.

No comments:
Post a Comment