Na Erick Nenda, OKULY BLOG, DODOMA
Wazee nchini wametakiwa kuacha kutafuta watu wa kulaumiwa kutokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii, badala yake wajitafakari na kujiuliza wajibu wao katika malezi ya watoto kuanzia ngazi ya familia ili kuimarisha jamii iliyokuwa imara na kujenga taifa.
Katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na kaundi maalum Mhe. Eliakim Maswi Amesema hayo Oktoba 1, 2026 wakati akizungumza na wawakilishi wa mabaraza ya wazee nchini katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani amesema kuwa wazee ni adhina la taifa letu.
Katika hotuba yake, Maswi amesema familia ni shule ya kwanza ambayo mtoto hujifunza maadili, heshima, ukweli, kufanya kazi, nidhamu, kuomba msamaha, kuwajibika na kuwa mkweli kabla hajafika shuleni kwa iyo wazee wanajukumu la kumjenga mtoto akiwa bado mdogo ili kuwezesha kuwa na maadili yaliyo mema kwa jamii.
"lengo la mkutano huu ni kufahamiana na ushirikiano wa kazi na kusikiliza hali halisi ya wazee katika kila mkoa na kukubaliana kwenye kulinda maadili na ushirikiano katika kuijenga jamii iliyokuwa nzuri na kuunganisha baraza na mwelekeo wa dira ya 2050," amesema maswi.
Amesema kuwa heshima kwa mzee haimaanishi kuwa mzee huyo yuko juu ya maadili, sheria au uwajibikaji, bali ni wajibu mkubwa kwake kuwa mfano mwema ndani ya familia na katika jamii kwa ujumla.
Maswi amesema wazee wana nafasi muhimu katika kujenga kizazi kinachozingatia maadili, akisisitiza kuwa malezi bora hayawezi kuachwa kwa wazazi pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa familia na jamii nzima.
Aidha, amewataka wazee kuendelea kushiriki katika malezi kwa kutoa ushauri na kuwa mfano wa kuigwa, huku wakizingatia mabadiliko ya wakati na mazingira ambayo vijana wanaishi na kuiboresha jamii nzuir ya kesho kwa taifa.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Wazee Duniani yamefanyika huku yakibeba kauli mbiu inayosema: Uzee na kuzeeka haukwepeki, uzee na kuchakaa haukubaliki" Kauli hiyo inalenga kuhamasisha jamii kutambua thamani ya wazee, kuwaheshimu na kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki katika maendeleo ya familia na taifa
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Taifa Mhe. David Sendo amesema kuwa wazee wamepambana sana kwenye kulifikisha taifa hapo lilipo kwa sasa na bado wanaendelea kujenga taifa zuri pamoja na hayo bado wazee awapewi kipaumbele kwenye baadhi ya maeneo.
Aidha, amesema kuwa bado wazee wamekuwa awapewi nafasi kwenye suala nzima la kufanya maamuzi katika serikali kundi hili limekuwa linaongezeka kwa kasi kwa sababu uzee ni wajibu kwa kila mtu hivyo wazee wapewe nafasi kijamii na kitaifa Maana wazee ni adhina kubwa.
"Kundi hili la wazee lenye kutoa ushauri wa hekima kwa taifa hivyo mzee asizalauliwe apate heshima anayostahili kwa ustamilivu wao wameweza kuhimili na kulinda uhuru na Amani tuliyokuwa nayo leo hivyo mahitaji yao yafanyiwe kazi," amesema Sendo.
Hata hivyo, wito umetolewa kwa jamii kutambua kuwa jukumu la malezi na ujenzi wa maadili ni la kila kizazi, huku wazee kutumia uzoefu wao kuimarisha maadili na mshikamano katika jamii na pia wazee kupewa kipaumbele kwenye suala la Afya na kupewa bima za afya ili kuwasaidia kupata huduma kwa wakati na usahihi.














No comments:
Post a Comment