SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AIPONGEZA REA UHAMASISHAJI NISHATI SAFI YA KUPIKIA VIJIJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 2, 2026

SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AIPONGEZA REA UHAMASISHAJI NISHATI SAFI YA KUPIKIA VIJIJINI


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ametembelea Maonyesho ya 50 Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ikiwemo banda la Wakala wa Nishati Vijini (REA) na kuipongeza REA kwa uhamasishaji wa wananchi katika matumizi ya nishati safi ya kupikia maeneo ya vijijini.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Julai 2, 2026 baada ya kupata taarifa za miradi pamoja na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na REA, Spika mtaafu Anna Makinda ameendelea kuhamasisha wananchi kutembelea banda la REA na kujifunza Teknolojia mbalimbali za nishati safi ya kupikia ili kuendelea kulinda mazingira pamoja na afya za wananchi.



No comments:

Post a Comment