TANZANIA YAZIDI KUN'GARA KIMATAIFA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA ,WATATU KUTOKA BURUNDI WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA NJIA YA MATUNDU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 10, 2026

TANZANIA YAZIDI KUN'GARA KIMATAIFA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA ,WATATU KUTOKA BURUNDI WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA NJIA YA MATUNDU



Na Boniphace John Epimack -Dodoma


Hospitali ya Benjamin Mkapa  (BMH)   imefanikiwa kufanya  kwa mara ya kwanza   upasuaji  wa moyo kwa njia ya matundu  kwa watoto watatu kutoka nchini Burundi ,hatua inayotajwa kuimarisha  uwezo wa Tanzania katika kutoa huduma za kibingwa na kukuza utalii wa matibabu  Barani Afrika.


Akieleza kuhusu mafanikio hayo leo Alhamisi ,julai 9,2026 hosiptalini hapo Jijini Dodoma ,Mkurugenzi mtendaji wa Hoslitali hiyo ,Profesa Abeli Makubi amesema Hatua hiyo inaendana na ajenda ya serikali ya kuendeleza utalii kwa kuvutia wagonjwa kutoka nchi jirani na mataifa mengine Duniani kupata huduma za kibingwa nchini Tanzania badala ya kusafiri nje ya afrika.


Profesa Makubi amesema Upasuaji huo wa watoto watatu  kutoka Burundi umefanywa  kwa ushirikiano kati ya wataalamu  wa  Hosipitali ya Benjamin  Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ikiwa ni sehemu ya juhudi  za  kujenga  uwezo wa ndani wa kutoa huduma za matibabu ya moyo nakupanua wigo wa huduma kwa wagonjwa kutoka nje ya nchi .


Ameongeza kuwa hapo awali huduma hiyo ilikuwa ikitolewa kwa watu wazima pekee ,lakini kutokana na kuimarika kwa uwezo wa hosipitali sasa imeanza kutolewa pia kwa watoto ambapo upasuaji huo umehusisha kuziba matundu  ya moyo kwa watoto wa tatu ,huku watoto wengine waliopimwa 

 wakipatiwa matibabu mbadala baada ya kubainika kuwa hali zao hazikukidhi vigezo vya kitaalamu vya kufanyiwa upasuaji huo na kutokana na ukubwa wa athari za ugonjwa.


Aidha amesema kuwa kuimarika kwa huduma hizo  kumepunguza idadi ya watanzania wanao lazimika kusafiri kwenda nje za nchi kufuata matibabu ya moyo.


Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka JKCI Godwin Sharao amesema utowaji  huduma kwa wagonjwa wa kimataifa huwapa wataalamu fursa ya kubaini maeneo yanayo hitaji maboresho nakuongeza ushindani wa kitaaluma .


amesema kuhudumia wagonjwa kutoka mataifa mengine kutasaidia kutaendelea kuboresha ubora wa huduma za matibabu Tanzania.











No comments:

Post a Comment