JUKWAA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LA TANZANIA–KOREA LATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 1, 2026

JUKWAA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LA TANZANIA–KOREA LATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI DODOMA


Seoul, Korea,

Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma imeendesha Jukwaa la Biashara na Uwekezaji (Trade and Investment Forum) 
lililokuwa na kaulimbiu ya Kuonesha Fursa lukuki zilizopo Mkoani Dodoma.

 Jukwaa hilo 
lilihusisha zaidi ya Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa 60, hususan kutoka katika jiji 
la kibiashara la Seoul.

Jukwaa hilo lililenga kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma na kuvutia 
wawekezaji katika sekta za Kilimo, Utalii na Ukarimu, Uchukuzi na Usafirishaji.

 Vilevile 
sekta za Viwanda na Biashara, Uchimbaji wa Madini, Huduma za maji, Usafi wa mazingira 
na Ujenzi wa Majengo na Miundombinu (Real estate).


Mgeni rasmi kwenye tukio hilo alikuwa ni Mhe. Dkt Ramadhani Rajabu Seif, Naibu Waziri, 
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Katika hotuba yake 
Mheshimiwa Naibu Waziri aliyakaribisha makampuni yaliyoshiriki kwenye Jukwaa hilo 
kuwekeza nchini Tanzania hususan, katika mkoa wa Dodoma, akiwahakikishia ushirikiano 
mkubwa kutoka serikalini.

“Tanzania ni nchi yenye utulivu na amani, mazingira mazuri na salama ya biashara na 
uwekezaji, hivyo tunawakaribisha sana kuwekeza katika nchi yetu,” alisema Mheshimiwa 
Seif.


Naye Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Mheshimiwa. Noel Kaganda aliwashukuru 
washiriki wa Jukwaa hilo kwa kukubali mwaliko na kujitokeza kwa wingi. 

Aidha 
aliwahakikishia wawekezaji kuwa Ubalozi utaendelea kutoa ushirikiano na taarifa za kutosha 
kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo ncini Tanzania ikiwemo katika Mkoa wa 
Dodoma, Mji Mkuu wa Tanzania.


Hali kadhalika Mheshimiwa. Rosemary Staki Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma 
alifafanua kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma kama vile kilimo 
cha Zabibu, Ufuta, Alizeti, Tufaa na Korosho. Pia alisisitiza juu ya vivutio mbalimbali 
vilivyopo mkoani Dodoma ukiwemo Utalii katika mbuga za Mkungunero na Swagaswaga; 
Utalii wa kihistoria hususan michoro ya miambani iliyopo Kondoa Irangi, utalii wa 
utamaduni; utalii wa mikutano; na michezo.

Vilevile, Mheshimiwa Senyamule alizungumzia fursa za uwekezaji katika sekta za uchukuzi 
na usafirishaji, hususan ujenzi wa reli za mijini kwa ajili ya kurahisisha usafiri katika jiji la 
Dodoma.

“Mkoa wa wetu unahitaji huduma hizi kwa sasa ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa wakazi 
wa Dodoma, ambapo ongezeko la watu linazidi kukua kwa kasi kubwa,” Alisema.

Pia Mkuu wa Mkoa alisisitiza uwepo wa fursa za biashara na uwekezaji katika sekta za 
viwanda na madini, ambapo mkoa wa Dodoma una zaidi ya aina 49 za madini adimu na ya 
kimkakati.

Kongamano lilikuwa na mawasilisho sita; ambapo mawasilisho matatu yalitoka Tanzania 
yakihusisha fursa za biashara na uwekezaji, mradi wa ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Hombolo 
(Hombolo Thematic Satellite City) na mradi wa ujenzi wa reli za mjini. Kwa upande wa Korea 
Kusini kulikuwa na mawasilisho matatu juu ya uzoefu wa uwekezaji wa Korea nchini 
Tanzania, na mazingira ya uwekezaji nchini.

 Wazungumzaji wa Makampuni hayo walikuwa 
ni: - Mtendaji Mkuu wa kampuni ya KFINCO, Mwenyekiti na Mtendaji mkuu wa Kmapuni 
ya KOIMA, Mwenyekiti wa Kampuni ya ICAK, Waziri wa Ardhi, Miundombinu na 
Uchukuzi (Mstaafu).

 Makampuni aliyotoa uzoefu ni KORAIL, HEELIM na Mwenyekiti wa 
Chama cha Wafanyabiashara wa Korea nchini Tanzania.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI KOREA
SEOUL

No comments:

Post a Comment