Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewasili mkoani Ruvuma leo, Julai 1, 2026, kwa ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, pamoja na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika ziara hiyo, Waziri Ulega anatarajiwa kutambulisha mradi wa ukarabati wa barabara ya Songea–Lutukira (kilomita 100) kwa kiwango cha lami, pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Songea Bypass (kilomita 16) kwa kiwango cha lami.
Miradi hiyo inatarajiwa kuboresha miundombinu ya usafiri, kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo, pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Ruvuma na maeneo ya jirani.









No comments:
Post a Comment