Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Donald Msengi pamoja na viongozi wengine wa Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa huo leo tarehe 03 Julai, 2026.
Waziri Ulega amefanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa huyo, ambapo amemueleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuimarisha miundombinu ya barabara ya Mtwara - Mingoyo (Mnazi Mmoja) - Masasi (km 201) na Mtwara - Tandahimba - Newala - Masasi (km 160) ili kuufungua Mkoa wa Mtwara na kuiunganisha na mikoa jirani ya Lindi, Pwani na Dar es Salaam kwa miundombinu ya Kisasa.










No comments:
Post a Comment