Na Mwandishi Wetu - MWANZA
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wameendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa na huduma zinazopatikana katika Sekta ya Madini kupitia maonesho yanayoendelea sambamba na Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026) jijini Mwanza.
Jukwaa hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini, wakiwemo makampuni ya uchimbaji wa madini, watoa huduma migodini, wafanyabiashara wa madini, wawekezaji, taasisi za umma na binafsi, pamoja na vyama vya wachimbaji wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini.
LCCF 2026 linafanyika chini ya kaulimbiu: “Kutoka Majadiliano hadi Utekelezaji: Kujenga Sekta Imara ya Madini kupitia Ushirikishwaji wa Watanzania na Uanzishwaji wa Viwanda.”











No comments:
Post a Comment