WAZIRI WA FEDHA ZIARANI NCHINI UINGEREZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 22, 2026

WAZIRI WA FEDHA ZIARANI NCHINI UINGEREZA


Na Benny Mwaipaja, London



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (MB), ameanza ziara ya kikazi ya siku sita jijini London, Uingereza, ambapo atashiriki katika matukio mbalimbali ikiwemo kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa hatifungani ya kwanza ya nje yenye sarafu ya Shilingi ya Tanzania inayotolewa na Shirika la Fedha la Kimataila (IFC) katika Soko la Hisa la London

Hatifungani hiyo inatarajiwa kupanua fursa za uwekezaji nchini na kuvutia aina mpya za wawekezaji wa kimataifa ambao wataunga mkono ajenda ya maendeleo ya muda mrefu ya nchi.

Mhe. Balozi Omar alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow, alilakiwa na Mwenyeji wake, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki, ambaye baadae Alasiri, alimkaribisha katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini London ambapo alipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi na baadae kujadili ajenda za ziara hiyo.

Ziara ya Mheshimiwa Balozi Omar inayoanza leo tarehe 21 hadi 26 Julai 2026, inalenga kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika masoko ya kimataifa ya fedha, kuvutia mitaji ya muda mrefu na kuithibitisha nchi kama moja ya maeneo yanayovutia zaidi uwekezaji barani Afrika.

Ziara hiyo pia inatoa fursa ya kufanya majadiliano na wasimamizi wa mali wa kimataifa, wawekezaji wa serikali, taasisi za uwekezaji wa maendeleo na benki za biashara kuhusu fursa zilizopo katika miundombinu, nishati, viwanda, kilimo, madini na huduma za kifedha.


Aidha, atashiriki mazungumzo ya pande mbili na washirika mbalimbali wa maendeleo na taasisi kubwa za kifedha duniani ikiwemo Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), Standard Bank na Soko la Hisa la London, kuhusu mwelekeo wa uchumi wa nchi, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 pamoja na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV).


No comments:

Post a Comment