Wizara ya Madini Yaahidi Kushirikiana na UAIT Kukuza Uongezaji Thamani Madini ya Vito - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 9, 2026

Wizara ya Madini Yaahidi Kushirikiana na UAIT Kukuza Uongezaji Thamani Madini ya Vito



Na Mwandishi Wetu - Dodoma


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, amekihakikishia ushirikiano Chuo cha United African Institute of Technology (UAIT) Cha Korea Kusini katika kuendeleza mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito kupitia Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Ahadi hiyo imetolewa Julai 9, 2026, jijini Dodoma, wakati wa kikao kati ya Naibu Katibu Mkuu na Mkuu wa Chuo cha UAIT, Prof. Chang Ki Lee.

Akizungumza katika kikao hicho, Mbibo amesema ushirikiano huo utaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu wengi wazawa wenye ujuzi wa kiwango cha juu katika shughuli za uongezaji thamani wa madini ya vito, hatua itakayochangia kuongeza thamani ya rasilimali za madini na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, viongozi hao wamejadiliana fursa mbalimbali za kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya Sekta ya Madini, mafunzo ya kitaalamu na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ushindani wa sekta hiyo nchini.

Kituo cha TGC kilichopo jijini Arusha, kinatoa mafunzo ya ngazi mbalimbali kwa muda mrefu na mfupi ya uongezaji thamani madini ya vito.





No comments:

Post a Comment