Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kipolisi Mtumba Jijini Dodoma Mrakibu wa Polisi Charles Mwamtobe (ASP), Charles Mwamtobe amezindua kampeni ya kuinua maendeleo ya wanafunzi pamoja n a uzalendo wa kutoa taarifa za uhalifu na uhalifu katika Wilaya hiyo.
Hayo yamejiri July, 31, 2026 katika shule ya Msingi Kikombo akiambatana na Polisi kata wa eneo ambapo amewataka wanafunzi kuwa wazalendo na kupaza sauti Kwa mamlaka husika pindi wanapoona viashiria vya vitendo vya uhalifu katika Jamii.
ASP, Mwantobe amesema wanafunzi wamekuwa na mchango mkubwa katika kuzuia vitendo vya kihalifu Kwa kutoa taarifa hivyo kamisheni ya Polisi Jamii imewatengenezea wanafunzi maziringira rafiki ya kutoa taarifa pamoja na kuwawezesha wanafunzi kitaaluma kupitia kampeni.
"Kampeni ya kalamu Moja mwanafunzi Moja arudi darasani itasaidia wanafunzi kuwa wazalendo na kuchukua uhalifu pamoja na kuongeze ufahulu wa wanafunzi katika Wilaya hiyo" ASP Mwantobe.
Uongozi wa shule ya Msingi Kikombo imetoka wito Kwa Jamii kuunga mkono Jeshi la Polisi kupitia kampeni hiyo iatakayo saidia ufaulu wa wanafunzi na taaluma.











No comments:
Post a Comment