Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameridhia ombi la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia tarehe 4 Septemba, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo Agosti 25, 2026, Rais Samia amepokea na kuridhia ombi hilo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais mwingine zitachukuliwa.
Taarifa imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, tarehe 25 Agosti, 2026.


No comments:
Post a Comment