Na. OWM - TAMISEMI, Dodoma
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali - TAMISEMI imeendelea kusogeza utoaji wa huduma ya elimu kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sekta za Uchumi na Uzalishaji Tawala za Mikoa Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Mhandisi Enock Nyanda amesema TAMISEMI inaendelea kusogeza huduma kwa wananchi sababu ni Wizara ambayo moja kwa moja huduma zake zinaenda kwa wananchi ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu, Kilimo na Miundombinu.
Amesema hayo leo Agosti 03, 2026 katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea viwanja vya John Malecela Jijini Dodoma.
" Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI ni miongoni mwa
Wizara za Mwanzo zilizoanzishwa mara baada ya kupata Uhuru mwaka1961 hivyo mengi mazuri yamefanyika katika kipindi chote, " ameeleza Mhandisi Nyanda.
Mhandisi Nyanda amebainisha hayo baada ya mwanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Gloria, iliyopo Ihumwa Jijini Dodoma,kuuliza Wizara ilianzishwa lini walipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.
Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea maonesho ya nanenane katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI pamoja na taasisi zake ikiwemo TARURA, DART, Shirika la Masoko Kariakoo, Tume ya Utumiwa wa Walimu, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo







No comments:
Post a Comment