WAZIRI KAPINGA AZINDUA KIWANDA DARASA CHA KUBANGUA KOROSHO MASASI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 11, 2026

WAZIRI KAPINGA AZINDUA KIWANDA DARASA CHA KUBANGUA KOROSHO MASASI

Na Mwandishi Wetu, Mtwara


Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amezindua kiwanda darasa cha kubangua korosho wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara, kilichojengwa na Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC), kwa lengo la kuongeza kasi ya ubanguaji wa korosho na kupunguza uuzaji wa korosho ghafi nje ya nchi.

Hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya zao la korosho na kuwawezesha wakulima kupata fursa zaidi za kunufaika na zao hilo, badala ya kutegemea kuuza korosho ghafi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Kapinga ameitaka CAMARTEC kuhakikisha teknolojia za kubangua korosho zinawafikia wakulima mmoja mmoja pamoja na wale waliopo katika vikundi, ili kuongeza uzalishaji na usindikaji wa korosho nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Mhandisi Godifrey Mwinama, amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kubangua hadi tani 700 za korosho kwa mwaka, hatua inayotarajiwa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa korosho zilizobanguliwa katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika teknolojia za kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa na wakulima wa mkoa huo.

Wakulima wa korosho pamoja na wabanguaji wamepongeza ujio wa kiwanda hicho, wakieleza kuwa ni hatua muhimu katika kuwasaidia wakulima wa Masasi kuongeza thamani ya korosho zao na kupata fursa kubwa zaidi za masoko.

Ujio wa kiwanda hicho ni sehemu ya juhudi za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, kukuza viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini na kuongeza kipato cha wakulima


No comments:

Post a Comment