Na Wellu Mtaki, Geita
Equity Bank Tanzania imeeleza kuwa inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wadau wa sekta ya madini, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha katika ununuzi wa mitambo na vifaa, pamoja na kugharamia shughuli za biashara katika mnyororo mzima wa thamani wa madini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Biashara kwa Wateja Wadogo, wa Kati na Binafsi wa Equity Bank Tanzania, Theresia Aloyce, wakati wa Maonesho ya Tisa ya Madini yaliyofanyika Geita.
Aloyce alitoa kauli hiyo baada ya Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, kutembelea banda la benki hiyo na kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa kwa wadau wa sekta ya madini.
Kwa mujibu wa Equity Bank Tanzania, huduma hizo zinalenga kuwafikia wadau mbalimbali wanaoshiriki katika sekta ya madini, wakiwemo wachimbaji, wafanyabiashara pamoja na watoa huduma zinazohusiana na shughuli za uchimbaji na biashara ya madini.
Benki hiyo pia inatoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi na mitambo inayohitajika katika shughuli za madini, sambamba na mikopo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika sekta hiyo.
Aloyce amesema huduma hizo hazilengi wachimbaji pekee, bali zinahusisha mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya madini, ikiwemo wafanyabiashara na wadau wengine wanaonufaika moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na shughuli za madini.
Aidha, viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kutumia fursa zilizopo katika sekta ya madini kwa ajili ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wanaoshiriki katika mnyoro wa thamani wa madini.
Katika tukio hilo, viongozi pia walitoa pongezi kwa washiriki na wadau mbalimbali kwa kushiriki katika maonesho hayo, huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za fedha na wadau wa sekta ya madini.
Equity Bank Tanzania imeahidi kuendelea kuboresha na kupanua huduma zake za kifedha ili kuwafikia wachimbaji, wafanyabiashara, wafanyakazi na wadau wengine wa sekta ya madini katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:
Post a Comment