MBUNGE wa Morogoro Kusini Mashariki Hamisi Shaban Taletale amesema mazoezi ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku na yana mchango mkubwa katika kupunguza na kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Hayo ameyasema Leo jijini Dar es salaam wakati akifanya mazoezi ikiwa ni kuelekea siku ya Maadhimisho ya Moyo Duniani ambayo huadhimishwa Kila Mwaka septemba 29 ambapo Taletale amesema ameyafanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yake kwa kufanya mazoezi kila siku huku akitumia siku za Jumamosi kuungana na wananchi wanaojitokeza kwa wingi kufanya mazoezi.
Amesema watu wanapaswa kuzingatia mazoezi hasa wanapofikia umri ambao mwili unahitaji kujengewa utaratibu wa mazoezi ili kuendelea kuwa na afya bora.
Ameongeza kuwa aina ya kazi zinazofanywa na baadhi ya viongozi na wabunge, ambazo zinahusisha kukaa kwenye viti kwa muda mrefu, zinaongeza umuhimu wa kuwa na muda maalumu wa kufanya mazoezi.
“Mazoezi yanasaidia kupunguza au kuzuia kabisa magonjwa yasiyoambukiza. Kwa hiyo ukipata nafasi ya kufanya mazoezi fanya sana,” amesema Taletale
Kwa Upande wake Happy Nchimbi - Meneja Mradi wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA)amesema siku ya wameamua kufanya mazoezi leo ikiwa ni kuadhimisha siku ya Moyo Duniani na kusema kuwa kwa kufanya mazoezi hayo kunaamsha uelewa kwa Wananchi juu ya Magonjwa yasiyoyakuambukiza na hususani Magonjwa ya Moyo.
Kwa upande wao wanafunzi Kutoka shule ya Sekondari zanaki walioshiriki mazoezi hayo Happiness Emanuel Na Joanita Felex wamesema mazoezi ni Muhimu kwao kwani yanasaidia kutokupata Magonjwa yasiyo yakuambuliza na kuweka Afya ya akili sawa

.jpeg)



No comments:
Post a Comment