MJUMBE WA KAMATI YA SIASA MARIAM MJEMA ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWANRI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 25, 2026

MJUMBE WA KAMATI YA SIASA MARIAM MJEMA ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWANRI





Same – Kilimanjaro

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Same, Mariam Mjema, ameshiriki katika mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, aliyewasili wilayani Same kuanza ziara ya kikazi.

Ndugu Mwanri amewasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Same, Jana ikiwa ni sehemu ya ziara yake iliyolenga kutembelea maeneo mbalimbali ya Majimbo ya Same Mashariki na Same Magharibi.

Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu huyo alikutana na viongozi na wanachama wa CCM, pamoja na wananchi, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za chama na maendeleo ya wananchi.


Mariam Mjema, akiwa miongoni mwa viongozi walioshiriki katika mapokezi hayo, amekuwa sehemu ya viongozi wa CCM wa Wilaya ya Same waliokuwepo kumpokea Naibu Katibu Mkuu huyo wakati wa kuwasili kwake.

Ziara hiyo hili hitimishwa kwa mkutano wa hadhara, ambapo Ndugu Mwanri alizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Same kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu chama na maendeleo ya jamii.

No comments:

Post a Comment