TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA GPE MULTIPLIER KUHAMASISHA UWEKEZAJI KATIKA ELIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 25, 2026

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA GPE MULTIPLIER KUHAMASISHA UWEKEZAJI KATIKA ELIMU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameshiriki mkutano wa GPE Multiplier Possibility wenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuimarisha elimu duniani, uliofanyika katika ECOSOC Chamber, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), New York nchini Marekani.

Mkutano huo umeongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Global Partnership for Education (GPE), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Mkutano huo umejikita katika juhudi za kutafuta na kuhamasisha rasilimali kutoka kwa wadau wa elimu duniani kupitia mfuko wa GPE, kwa lengo la kusaidia nchi wanachama kuimarisha na kufadhili miradi mbalimbali ya elimu.

Kupitia mpango huo, wadau wa elimu duniani wanahamasishwa kutoa michango itakayowezesha kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, hususan katika maeneo yanayohitaji rasilimali zaidi kwa ajili ya kuboresha upatikanaji na ubora wa elimu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazowanufaika na ufadhili wa Global Partnership for Education (GPE), unaolenga kusaidia nchi katika kuimarisha mifumo ya elimu na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ya elimu.

No comments:

Post a Comment