• Yapokelewa kwa shangwe Geita, wananchi waahidi kujiunga
Kifurushi cha Umoja Afya cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kimepokelewa kwa shangwe na wananchi wa Mkoa wa Geita wakiweka wazi kuwa ni mkombozi wa kulinda afya, kipato na mitaji ya wajasiliamali. Kifurushi hicho ambacho kinawalenga wananchi waliojiunga kwenye vikundi kuanzia vya watu 10 na kuendelea kikiwa na gharama ya Shilingi 60,000 kwa kila mwanakikundi kitawapa fursa ya kujiunga na kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.
Hatua hiyo imejionesha katika Kongamano la Wajasilimali lililofanyika katika Maonesho ya Madini Mkoa wa Geita ambapo wameonesha kuvutiwa na Kifurushi hicho huku baadhi yao wakipongeza uwepo wake na kuahidi kujiunga ili kujilinda dhidi ya gharama za matibabu zinazoweza kuathiri mitaji yao na ustawi wa familia.
Akizungumza katika kongamano hilo, Meneja wa NHIF Mkoa wa Geita, Bi. Sophia Kaku, amesema kuwa bima ya afya ni nyenzo muhimu ya kulinda afya na kipato cha wananchi, hususan wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji madini na biashara ndogondogo ambazo zina changamoto mbalimbali za kiafya.
Amesisitiza kuwa dhana ya utajiri endelevu haiwezi kutenganishwa na afya bora, akieleza kuwa, bima ya afya inamwezesha mwananchi kupata huduma za matibabu bila kulazimika kutumia fedha alizotenga kwa ajili ya kuendesha biashara au shughuli nyingine za kiuchumi.
“Uchimbaji madini una changamoto zake za kiafya, hivyo ni muhimu kwa wachimbaji na wananchi wengine kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wanapozihitaji. Bima ya afya ni ulinzi wa afya zetu, mitaji yetu na familia kwa ujumla,” alisema Bi. Kaku.
Alifafanua kuwa kupitia Kifurushi cha Umoja Afya, NHIF imetoa fursa kwa vikundi vyenye watu kuanzia 10 kujiunga kwa gharama ya Shilingi 60,000 kwa kila mwanachama kwa mwaka, hatua inayorahisisha upatikanaji wa huduma za bima ya afya kwa wananchi wenye kipato cha kawaida.
Aidha, alisema kifurushi hicho kinawezesha wananchi kuwaunganisha hata ndugu zao katika kundi la watu 10, hivyo kurahisisha mchakato wa usajili na kuwapa fursa ya kulinda afya zao kwa pamoja.
Bi. Kaku alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo kwa kujiunga na Umoja Afya, akibainisha kuwa juhudi za kupanua wigo wa bima ya afya zinaendana na dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata ulinzi wa kiafya.
Akizungumzia utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, alisema Ofisi ya NHIF Mkoa wa Geita inaendelea na usajili wa kaya zisizo na uwezo ambazo gharama za kifurushi cha Shilingi 150,000 kwa mwaka zinagharamiwa na Serikali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha makundi yenye uhitaji yanapata huduma za afya.
Vilevile, alieleza kuwa NHIF imeendelea kurahisisha mifumo ya usajili kwa kuiunganisha na mifumo mingine ya utambuzi, hatua inayomwezesha mwananchi kujiunga na Mfuko bila vikwazo vya mahali alipo.
Mifumo hiyo pia inawezesha wanachama kufuatilia matumizi ya huduma zao na kuimarisha udhibiti wa vitendo vya udanganyifu.
Kwa upande wao, wananchi walioshiriki katika kongamano hilo walipongeza jitihada za NHIF za kuanzisha Kifurushi cha Umoja Afya, wakieleza kuwa ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao mara nyingi hukabiliwa na changamoto ya kugharamia matibabu bila kuathiri mitaji yao.
Walisema uwepo wa kifurushi hicho utawasaidia kupata uhakika wa huduma za matibabu, kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kulinda ustawi wa familia zao, huku wakiahidi kuhamasisha wenzao kujiunga.
Aidha, kupitia maonesho hayo, NHIF imeendelea kutoa huduma za elimu kuhusu bima ya afya pamoja na upimaji wa afya kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kujikinga dhidi ya athari za kiafya na kifedha.
Maonesho ya Madini 2026 yamekuwa fursa muhimu kwa NHIF kuwakutanisha wananchi na wataalamu wake, kueleza huduma zinazotolewa na kutoa elimu kuhusu namna bima ya afya inavyoweza kuwa nyenzo ya kulinda afya, mitaji na maendeleo ya kiuchumi.

No comments:
Post a Comment