CCM YAZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE CHAMWINO, NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 16, 2026

CCM YAZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE CHAMWINO, NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO.



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki ufunguzi wa Kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Nettho Ndilito, zilizofanyika katika Kijiji cha Dabalo Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 16 Oktoba 2026.

Katika ufunguzi wa kampeni hizo, Mhe. Ndejembi amewasihi wananchi wa Jimbo la Chamwino kumchagua kwa kishindo Dkt. Ndilito, ili aweze kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika jimbo hilo hususani huduma za kijamii kama vile maji, umeme, miundombinu ya barabara, shule, vituo vya afya na zahanati.

Amesema kupitia Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetekeleza miradi muhimu ya huduma za kijamii katika jimbo hilo, hivyo shukrani pekee zinazofaa ni kumchagua Dkt. Ndilito ili aendelee kuisimamia vema Ilani ya CCM katika Jimbo hilo.

Mhe. Ndejembi amewataka wagombea wote walioshiriki mchakato wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi kuungana kwa pamoja na wana CCM wengine kuhakikisha Dkt. Ndilito anapata ushindi wa kishindo.

Makamu wa Rais Mhe. Ndejembi ambaye awali alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo, amewaahidi wananchi wa Chamwino kuendelea kushirikiana nao vema kuhakikisha jimbo hilo linapata maendeleo yaliyokusudiwa.

Amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jimbo hilo, huku akiwasisitiza wananchi wa Jimbo hilo kuendelea kumuombea Mhe. Rais katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Ndejembi ametumia nafasi hiyo, kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Chamwino kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichohudumu akiwa Mbunge wa Jimbo hilo. Amesema daima anathamini mchango wa kila mwananchi wa Chamwino alioutoa kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Hafla ya uzinduzi ya wa Kampeni za Ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia CCM, zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Wabunge, Madiwani na Wananchi mbalimbali.




No comments:

Post a Comment