DKT. MWIGULU ATAKA MADINI ADIMU YAONGEZEWA THAMANI NCHINI TANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 8, 2026

DKT. MWIGULU ATAKA MADINI ADIMU YAONGEZEWA THAMANI NCHINI TANZANIA



Na Mwandishi Wetu - London, Uingereza



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza umuhimu wa Tanzania kuendelea kuwekeza katika matumizi ya teknolojia ya kisasa na utaalamu wa ndani utakaowezesha nchi kuongeza thamani ya madini adimu (critical minerals) badala ya kuyauza katika hali ghafi kwenda nje ya nchi.

Akipokea ripoti ya utafiti kutoka kampuni ya McKinsey ya Uingereza mjini London, Dkt. Mwigulu alieleza kuwa rasilimali hizo zinapaswa kuwa kichocheo cha uchumi na viwanda vya ndani.

Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo kwenye teknolojia na tafiti ili kukuza ajira na pato la taifa.

Msimamo huu unaendana na mikakati ya Wizara ya Madini na Mkakati wa Miaka Mitano (2026/27–2030/31) unaolenga kupunguza usafirishaji wa madini ghafi.

Miradi inayotarajiwa kunufaika ni pamoja na Kabanga Nickel, Ngualla, Graphite ya Lindi na Mahenge, na Sotta Uranium, wakati serikali ikiendelea kuboresha miundombinu kama nishati, SGR na mifumo ya kodi.

No comments:

Post a Comment